Breaking: Ajali Yateketeza Maabara Sekondari ya Geita
AJALI mbaya imetokea usiku wa kuamkia leo Jumatano, Julai 7, 2021, baada ya moto kulipuka katika jengo la maabara ya Biology katika Shule ya Sekondari Geita (GESECO) mkoani Geita na kuteketeza jengo hilo na vifaa wanafunzi vilivyokuwemo ndani yake.
Ajali hiyo imetokea ikiwa ni siku moja tu baada ya kuibuka moto kwenye chumba cha kuhifadhia vifaa vya wanafunzi katika shule hiyo.
Hakuna maafa ya vifo au majeruhi walioripotiwa kutokana na ajali hiyo. Hata hivyo wanafunzi wachache walikuwa wamelala katika mabweni yao wakati tukio hilo likitokea wakati wengi wao bado hawajarejea kutoka likizo.
Aidha, Jeshi la Polisi Kikosi cha Zimamoto wapo eneo la tukio lakini bado hawajatoa tamko lolote kutokana na ajali hiyo, hivyo mpaka sasa chanzo cha moto huo hakijaelezwa wala hasara iliyosababishwa na moto huo.
Taarifa Zaidi kutoka eneo la tukio, endelea kuwa karibu na #GlobalPublishersUpdates na Global TV Online.
No comments