Header Ads

Header ADS

Tanzania na Marekani zaahidi kuboresha mahusiano, Marekani yathibitisha



Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan Jumanne hii amefanya mazungumzo na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken , mazungumzo yaliyojikita zaidi kwenye masuala ya ugonjwa wa Covid-19, Demokrasia na mazingira ya kufanya biashara Tanzania.



Katika mtandao wake wa Twitter, Blinken amesifu jitihada za Rais Samia katika kukabiliana na janga la Corona.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu ya Tanzania, Bwana Blinken amesifu pia jitihada za Rais Samia katika kuimarisha demokrasia na azma yake ya kukutana na kushirikiana na vyama vya siasa pamoja na kusimamia uhuru wa vyombo vya habari.

Hata hivyo Chama kikuu cha Upinzani nchini humo (CHADEMA), kinaeleza kwamba hakijataarifiwa rasmi ni lini Rais huyo atakutana nao, licha ya maombi yao ya kuonana nae yalikubaliwa.

Kwa sasa joto la kisiasa nchini humo limejielekeza kwenye kupatikana kwa Katiba mpya, ambapo mbali na wanaharakati na makundi mengie, vyama vya siasa nchini humo vimekuwa vikipiga kelele kutaka Katiba mpya ya nchi hiyo, kufuatia mchakato wake kusimama kwa zaidi ya sita.

Rais Samia hivi karibuni alisema apewe muda kwanza kuhusu katiba mpya kwa kuwa anajenga uchumi wa nchi hiyo kwa sasa.

Mbali na hilo, na kuhaidi kwamba Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na Serikali ya Marekani, taarifa yaIkulu ya nchi hiyo inasema Rais Samia ametoa mwaliko kwa Rais Joe Biden wa Marekani kutembelea Tanzania ili kuimarisha zaidi uhusiano baina ya nchi hizo.

I had a productive conversation with Tanzanian President Hassan today. Our partnership is strong and enduring, and together we are working to ensure a peaceful, prosperous future for all Tanzanians – this includes our continued cooperation to fight the COVID-19 pandemic.

— 


No comments

Powered by Blogger.