Milioni Moja Yawatokea PUANI Watu Watatu, ni Baada ya Kutoka Kumuozesha Mwanafunzi wa Darasa la Sita
Wakazi watatu wa Wilaya ya Tanganyika wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kula njama ya kumuozesha Mwanafunzi wa Darasa la 6 kwa mahari ya Tsh. Milioni 1
Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Benjamin Kuzaga amethibitisha kukamatwa kwa watu hao wakiwemo Baba wa Kambo, Mama wa Mwanafunzi huyo pamoja na Balozi wa Mtaa wa Idoselo
Ameeleza kuwa, Januari mwaka huu watuhumiwa hao walikutana kupanga mahari na baada ya kikao Binti (16) aliitwa na kuelezwa mipango ya kuolewa. Mwanafunzi huyo hakukubali na Mama yake alimfukuza nyumbani
Kamanda Kuzaga amesema Watuhumiwa wote watafikishwa Mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika
No comments