Mzazi Aliyegoma Kuwapeleka Watoto SHULE Kisa Dini Hairuhusu Akamatwa na Polisi
Merchades Mugishagwe anashikiliwa na Polisi kwa Amri ya Mkuu wa Wilaya ya Bukoba akidaiwa kukaidi agizo la kuwaandikisha Watoto wake watatu Shule
Wakati Mzazi huyo akikamatwa, Serikali imewapeleka Watoto hao Shule ambapo Mtoto mkubwa (13) ameandikishwa Darasa la Nne, mwenye miaka 9 ameandikishwa Darasa la Pili huku mdogo wa miaka mitano akiandikishwa Darasa la Awali
Watoto hao wamepelekwa Shule chini ya usimamizi wa Halmashauri wa Manispaa ya Bukoba baada ya Serikali Wilaya ya Bukoba kuingilia kati uamuzi wa Wazazi wa kutowapeleka Shule kwasababu imani yake haiamini katika #Elimu ya Dunia.
No comments