Stars yanogesha dili la Fei Toto, TP Mazembe
DILI la kujiunga na TP Mazembe ya DR Congo, la kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ limenoga zaidi huko Yanga, ambapo taarifa zimeeleza kuwa tayari viongozi wa klabu hiyo wameshawasilisha dau na kumnasa kwenye dirisha la usajili lijalo.
Mazembe wamezidi kuvutiwa na uwezo wa Fei Toto kiasi kwamba sasa wanasuburia tamko la Yanga tu ili waweze kumwaga pesa.
Chanzo kimeeleza kuwa hatimaye sasa Mazembe wameamua kuleta ofa maalumu kwa uongozi wa Yanga kuhusu kumsajili Fei.
“Ama kweli kila lenye mwanzo huwa halikosi mwisho, kwani pamoja na kuwepo na tetesi nyingi kiasi cha baadhi ya watu kubeza juu ya dili hilo, nikueleze tu kwamba mechi ya Stars imeongeza chachu ya TP Mazembe kumtaka Fei Toto.
“Kwani kilichobaki sasa ni kwetu viongozi kukubaliana juu ya ofa yao ili nasi tuweze kufaidi matunda ya kuuzwa kwake, TP Mazembe wametoa dau la Sh milioni 200 ili wavunje mkataba wake, ila sisi tunadhani wanatakiwa kuongeza hadi ifike Sh milioni 300 na kitu hivi ili tuwapatie jembe letu,” kilisema chanzo hicho.
Feti Toto alionyesha uwezo wa juu kiasi cha kuwavutia wengi katika mchezo wa Jumanne ya wiki hii dhidi ya Tunisia, ambapo alifunga bapo la kusawazisha la Stars mchezo ukimalizika kwa sare ya bao 1-1.
No comments