Header Ads

Header ADS

Kutimuliwa Sauz! Uchebe Afunguka Kilicho Nyuma ya Pazia




BAADA ya aliyekuwa Kocha wa Simba, Patrick Aussems kutimuliwa ndani ya kikosi cha Black Leopards kinachoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini, amevunja ukimya na kuweka bayana chanzo cha kudumu kwa miezi mitatu pekee kwenye timu hiyo.

Aussems maarufu kwa jina la Uchebe amesema kuwa watu wamekuwa wakitafsiri vibaya chanzo cha yeye kuondoka kwenye timu hiyo na kudai kuwa hakufutwa kazi na badala yake aliamua kuondoka mwenyewe kutokana na kutoridhishwa na mazingira ya klabu hiyo.

Kupitia ujumbe alioweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, Aussems alieleza: “Wacha tuwe wazi. Hatuzungumzii juu ya kufutwa kazi, kujiuzulu au kutimuliwa kazi.

“Mnamo Septemba nilipata ofa rasmi kutoka kwa klabu, nilikuja Afrika Kusini kuangalia lakini kile nilichokiona kwa klabu kwa wiki sita hakikunifurahisha hata kidogo.

“Maono yetu yalikuwa tofauti sana! Kwa hivyo sikuwa na hamu tena na ofa hiyo na kwa hivyo sikusaini mkataba na nikaondoka, ni rahisi tu! Kwa hivyo, nawatakia kila la heri!”

Mbelgiji huyo ambaye alipata umaarufu mkubwa akiwa na kikosi cha Simba, baada ya kuwapa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, FA na kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akiwa ndani ya Black Leopards, kacheza michezo mitatu na kufungwa yote.

Kwa sasa Leopards ipo katika mikono ya kocha mwingine aliyewahi kupita Simba Dylan Ker, aliyetangazwa kurithi nafasi hiyo muda mfupi baada ya Uchebe kufutwa kazi.

Mwandishi Wetu,

Dar es Salaam




No comments

Powered by Blogger.