Wafungwa 44 watoroka gerezani Lebanon
Nchini Lebanon, polisi inawasaka wafungwa 44 waliotoroka katika gereza lililopo kwenye viunga vya jiji la Beirut, na hivyo kuwataka raia kuwa katika hali ya tahadhari.
Pamoja na kuwepo kwa ulinzi mkali watu 69 walilivunja jengo ambalo walikua wanazuiliwa lililopo karibu na makazi ya rais ya Baabda, mashariki mwa Beirut.
Kwa mujibu wa polisi, watano miongoni mwa wafungwa hao walikufa baada ya gari waliloiba wakati wakitoroka kupoteza uelekeo na kugonga mti.
Majeruhi mwingine alipelekwa hospitali. Taarifa ya polisi ilisema mapema mchana wa leo waliweza kuwatia nguvuni wafungwa 15, na wengine wanne walirejea wenyewe gerezani, wakisalia hao 44 wasikojulikana walipo.
No comments