Header Ads

Header ADS

Msanii wa filamu Asha Boko aolewa kwa mara pili

  


Msanii wa filamu wa muda mrefu hapa nchini Tanzania Asha Boko siku ya leo Novemba 20, ameweza kufunga ndoa kwa mara ya pili na mume wake Duwa Msafiri huko nyumbani kwao Mlandizi.

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital amesema hakutaka ndoa yake ijulikane kwa sababu watu wangeweza kutia vizuizi isitokee na kesho watafanya sherehe ukumbini maeneo ya Bagamoyo.


"Ni kweli nimeolewa leo nyumbani kwetu Mlandizi, mume wangu anaitwa Duwa Msafiri na kesho kutakuwa na sherehe ukumbini maeneo ya Bagamoyo, nilikuwa sijatangaza kwa sababu nisingeolewa watu wangenitangaza ila taarifa nimetoa kwenye familia, ndugu, jamaa na marafiki, mume wangu sio mtu maarufu hawawezi kumuiba kwa sababu anajielewa" amesema Asha Boko


Asha Boko amefunga ndoa hiyo ikiwa ni mara yake ya pili baada ya mume wake wa kwanza kushambuliwa na majambazi hadi kufariki mwaka 2010 wakati walipovamiwa nyumbani kwao Kimara, Jijini Dar Es Salaam.



No comments

Powered by Blogger.