Watatu Wahukumiwa Kwa Kuisababishia Hasara TANESCO
Watu watatu wamehukumiwa kwenda jela miezi sita au kulipa faini ya laki mbili kwa kila mmoja kwa kosa la kulisababishia shirika la umeme Tanesco hasara ya zaidi ya milioni 15.
Watu hao ni Gaston Masika, Gerald Constantine, Freeman Shirima, ambao wamekiri kutenda kosa hilo baada ya kusomewa shtaka linalowakabili mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Cassian Matembele, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam.
Hakimu Matembele, amesema kwa kuwa washtakiwa hao wamekiri kutenda kosa hilo na kuingia makubaliano na Serikali ambapo wametakiwa kulipa fidia ya shilingi milioni 15,803,000.
Washtakiwa hao wanadaiwa kati ya Februari 2016 na Agosti 2020 katika eneo la Mwenge barabara ya Sam Nujoma, Jijini Dar es salaam kwa kukusudia waliingilia mita ya Tanesco na kuisababishia hasara ya milioni 15,803,000.
No comments