Gigy Money aitwa kuombewa na mtumishi wa Mungu
Mtumishi wa Mungu na msanii wa zamani wa filamu Asnath Mathias amesema anatamani kumuombea msanii Gigy Money kutokana na vitu vyake vya ajabu anavyovifanya mitandaoni na jinsi anavyozungumziwa kwa watu.
Mtumishi huyo wa Mungu amesema Gigy Money ni mwanamke mzuri sana ila hapendezewi na maisha aliyokuwa nayo na amemshauri amuombee ili aanzishe maisha mapya, atulie na ajiheshimu.
"Kuokoka sio kuwa na shida na mtu bali ni kuacha mambo ya kidunia na kufanya kitu ambacho kitampendeza Mungu, Gigy Money ni mwanamke mzuri mno atambue hilo lakini ukifungua mitandao lazima utamuona na unaona vitu vya ajabu ambavyo anavifanya na watu wanavyomzungumzia" amesema
"Anaweza akaanzisha maisha yake mapya ili atulie, ajiheshimu na aijue thamani yake kama mzazi na mwanamke, anaweza asiamini ila naweza kumuombea kwa Mungu kumpa neema ya kubadilika" ameongeza
Aidha amesema anatamani kuwaona wasanii wa BongoFleva kama Lady Jaydee na Ruby kuimba nyimbo za Injili kwani zinawafaa na zitawapendeza.
No comments