Watu wasiojulikana wamchukua kiongozi wa maandamano Belarus
Kiongozi wa maandamano nchini Belarus Maria Kalesnikava amechukuliwa na watu wasiojulikana waliovalia barakoa na kumtia kwenye gari katika eneo la katikati ya mji mkuu Minsk.
Belarus Opposition Leader Maria Kalesnikava Abducted By Masked Men - The Women Journal
Ripoti za kuchukuliwa kwa kiongozi huyo wa maandamano imetolewa na shirika moja la habari la kujitegemea linaloitwa Tut, lililosema limeipata taarifa hiyo kupitia chanzo kimoja. Tukio hilo linadaiwa kutokea leo Jumatatu asubuhi na hakuna mtu yoyote aliyefanikiwa kuwasiliana na Kalesnikava.
Chanzo cha habari kimesema hakikuweza kurekodi tukio hili kwa simu yake kwa sababu alihofia naye kukamatwa. Kalesnikava mwenye umri wa miaka 38 ni mshirika mkubwa wa kiongozi wa upinzani wa Belarus Svetlana Tikhanovskaya na amekuwa akiongoza maandamano baada ya kiongozi wa upinzani kukimbilia nchi jirani ya Lithuania.
Kalesnikava pia ni mwanachama wa baraza la uratibu la Tikhanovskaya linalotaka yafanyike mazungumzo kwa ajili ya kipindi cha mpito cha kugawana madaraka nchini Belarus.
No comments