Young Lunya kamtaja Country Boy kama ndiyo Father of new Generation
Last Friday kwenye Jiwe La wiki la XXL ya Clouds FM ilisimama ngoma ya ‘Serikali Kuu ya Mizuka’, moja kati ya wimbo ambao unafanya poa sana kwasasa, Huku mtaani taarifa ziko dai kuwa mpaka sasa Young Lunya anastahili kuwa father of New Generation, huku kwa upande wake yeye anaamini yupo ambaye Ndio Father Of New Generation.
Sasa leo June 9, 2020 kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM Young Lunya amefunguka na kumtaja Country Boy kuwa anastahili kuwa father of new Generation.
“Unajua Country Boy ameanza miaka Tisa nyuma, alikuwa anafanya muziki huu ambao umepata nafasi mara ya kwanza ulikuwa muziki ambao hauwezi kupewa nafasi radioni, ameupigania mpaka leo tunaona kweli muziki umeenda huo watu wanaufanya, kwahiyo yeye kwakua ameanza Muda mrefu miaka Tisa nyuma anahaki ya kuwa father of this new generation na anaonekana anafanya kazi, anajuhudi” – Young Lunya
No comments