Header Ads

Header ADS

Lori Bado Halijatolewa Wami Kisa Milioni 5 “Maiti Haijasafirishwa, Sina Pesa, Nalala nje Polisi”



Mwajuma Selemani ni Mmiliki wa Lori ambalo limezama Mto Wami na kuua Dereva (Frank) ambaye  mwili wake umeopolewa baada ya kukaa chini ya maji kwa zaidi ya siku tatu, amesema bado Lori hilo halijatolewa ndani ya maji kwakuwa wenye uwezo wa kutoa wanataka hadi zipatikane Tsh. Millioni tano, na yeye ameishiwa pesa hivyo uwezo wa kulipia Million 5 hana.

“Dereva wangu amefariki, Makondakta wapo Hospitali nagharamia mimi, gari ina bima ndogo na ni gari pede nilikuwa nayo baada ya kujichanga sana ndipo nikainunua nikiamini itaniingizia kipato lakini safari ya kwanza ndio hii imezama Mtoni, maiti haijazikwa unasubiriwa mchango wangu, nipo Wami siku zaidi ya nne nalala nje kituo cha Polisi”– Mwajuma

No comments

Powered by Blogger.