Header Ads

Header ADS

Tekashi 69 Amvua Nguo Meek Mill LIVE Instagram " Nick Minaj Ndio Aliyekupa Umaarufu"


Tekashi 69 amefanya kama desturi sasa, kila aachiapo wimbo basi hutafuta kisusio cha kusindikizia. Jana aliidondosha "Trollz" kolabo yake na Nicki Minaj, kisusio kilikuwa Meek Mill.

Rapper huyo mtata alienda LIVE kwenye instagram yake akiitambulisha ngoma yake na baadaye alihamia kwa Meek Mill na kuanza kumsasambua kwamba alikuwa chawa tu wa Nicki Minaj, na Nicki ndiye aliyemtambulisha kwenye muziki. Awali alikuwa akizunguka tu kwenye matamasha ya Nicki na kufanya utangulizi wa show
-
"Nageukia kwa Meek Mill sasa, Sikiliza Nicki alikuchukua na kuzunguka naye kwenye ziara. Ulikuwa mtangulizi tu kwenye show zake. Nicki amekutengeneza, hakuna aliyetaka kuwa na wewe. Hivi umesahau ulivyokuwa? Sikia Nimesahau ambacho Drake aliwahi kusema, kitu kama hiki kwamba 'Hii ni ziara yako au ya mpenzi wako.' hiyo haikuwa ziara yako mshkaji wangu, sikia umewekwa kwenye ramani na Nicki Minaj. Hakuna aliyekuwa anakufahamu." alisema 69.

Yote hayo yamekuja baada ya Meek Mill kumuita Tekashi 69 panya 'rat' kwa kuwasaliti wenzake. Wakati akizungumza LIVE, Tekashi aliweka picha ya Meek Mill, Jay-Z na Desiree Perez ambaye ni CEO wa Roc Nation aliyeshtakiwa kwa madawa ya kulevya miaka ya 90 lakini aliachiwa huru baada ya kushirikiana vyema na vyombo vya dola.

Sasa Tekashi anamuuliza Meek Mill, "Unaniita mimi panya, mbona wewe pia unaongozana na panya kila siku?" akimuhusisha Perez.
1d

No comments

Powered by Blogger.