Header Ads

Header ADS

RC Aukataa Ubunge, Adai Yeye Anatafuta Kura za JPM


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema kuwa wakati anapewa nafasi hiyo aliambiwa akachape kazi hivyo ni lazima atekeleze agizo hilo kwanza na wala hana hata mpango wa kupanga foleni kutafuta jimbo wa Ubunge wa Viti Maalum.


RC Mndeme ametoa kauli hiyo leo Juni 23, 2020, kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio, wakati akieleza majukumu yake katika Mkoa na kusema kuwa kitu cha kwanza ambacho amekuwa akikizingatia ni masuala ya usalama kisha mambo mengine ndiyo yanafuata.

"Mimi nachapa kazi sababu nimetumwa kuchapa kazi, sijatumwa kugombea mimi mtaniona kwenye harakati natafuta kura za Rais Magufuli na wana CCM, Madiwani na Wabunge lakini siyo kugombea Jimbo wala Ubunge wa Viti Maalum" amesema RC Mndeme.


No comments

Powered by Blogger.