Vanessa Mdee "Wasanii Wenzangu Wamenishukuru Kwa Kufunguka Ukweli Kuhusu Tasnia ya Muziki"
Vanessa alitangaza kujitoa katika tasnia ya muziki wiki iliyopita kupitia ‘podcast’ yake akidai ilimpelekea kupata msongo wa mawazo
Vanessa ambaye sasa anaishi nchini Marekani na Mpenzi wake Rotimi ambaye ni msanii wa filamu na muziki kutoka Nigeria amesema tasnia ya muziki imejaa mambo yasiyofaa yanayopelekea matatizo kwa afya ya akili hususan kwa wasanii wa kike
Ameeleza kuwa maisha ya wasanii hayana uhalisia kwani wanalazimika kuendana na ukubwa wa brand zao hata wanapokosa uwezo huo
Katika kuonesha kiasi cha msongo wa mawazo alichopitia amekiri kuwa alikuwa analazimika kulewa kila anapotaka kulala kwa kipindi cha mwaka 2019 wote
Vanessa ameshukuru kwa maisha kumpa nafasi ya pili kupitia kukutana kwake na Rotimi na ameeleza ukweli huo ili kujiweka huru yeye, mashabiki wake na mabinti wengine
No comments