RC Homera Ameliagiza Jeshi la Polisi Kuwafikisha Mahakama Waliohusika Kupotea Maiti Mbili za Vichanga
Mkuu Wa Mkoa Wa Katavi Juma Homera amelipa siku saba Jeshi la Polisi kuwafikisha mahakamani watumishi wa hospitali waliohusika kupotea kwa maiti mbili za vichanga.
“Haiwezekani maiti za vichanga hao zikosekane wakati wasimamizi wa chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo wapo wasimamishwe kazi wakati upelelezi ukiendelea,”
Alisema hakuna haja ya kuendelea kukaa na watu wanaosababisha shida katika idara.
“Kwanini maiti hizo zipotee na hatujui zimeenda kufanyiwa nini,” alihoji Homera
Aliongesea kuwa “Hatuwezi kusubili mtu mwingine aje atatuwe matatizo ya katavi wakati kuna mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya na viongozi wengine,inaonekana kuna watu wanadanganywa ukifanya hivyo utashinda uchaguzi,au utapata madini mengi!na huu mchezo unaonekana ulikuwepo,”alisema Homera.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Mkoa wa Katavi, Dk Justina Tizeba alisema siku ya tukio alipokea taarifa kutoka kwa Muuguzi mfawidhi kuwa kuna tatizo limejitokeza la kupotea kwa maiti mbili.
Alisema alipofika waliwahoji wahusika wa chumba cha kuhifadhia maiti walikiri kupokea maiti hizo na kudhihifadhi.
Wafanyakazi hao wamedai kuwa wakati wa kuzitoa ili kuwakabidhi wahusika hazikuonekana.
Dk Tizeba alisema walitoa taarifa kituo cha polisi na wahusika walikamatwa na kupatiwa dhamana.
No comments