Rais wa La Liga afunguka Mtazamo Wake Kuhusu Ushirikiano na yanga
RAIS wa Kampuni ya La Liga ya Hispania, Javier Tebas ameeleza jinsi La Liga inavyoutazama ushirikiano huo kwa manufaa makubwa.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Tebas amesema Mkataba huo na Mabingwa wa Kihistoria na Kampuni ya GSM kama wadhamini ni mwanzo mzuri kwa La Liga kuonyesha uwezo wale katika kubadili na kuleta changamoto mpya ya maendeleo kwenye soka la Afrika.
"Kupiga chapuo uendeshaji wa kiweledi kwa soka la Afrika na Duniani kote ni dhima tulizonazo kama La Liga katika mkakati wa kujitanua kimataifa. Mkataba huu tuliosaini na GSM na Yanga ni mwanzo mzuri kwetu,” amesema Rais huyo wa LaLiga.
"Tunajivunia sana kuhusika katika maendeleo ya klabu ya Yanga kwa sababu huduma hii ya ushauri tunayokwenda kuipa Yanga inakwenda kuwa ya manufaa makubwa," amesema.
No comments