Nyota ya Rais Trump Kwenye Hollywood Walk of Fame Yaharibiwa Waacha Kinyesi Cha Mbwa
Juzi (June 8) Nyota ya Rais Donald Trump kwenye Hollywood Walk of Fame iliharibiwa vibaya kwa kuchorwa kwa juu na rangi nyeusi na kuandikwa ujumbe wa 'Black Lives Matter' na pia mtu mmoja kuacha kinyesi cha Mbwa kwenye mfuko katikati. SWIPE
Huu ni muendelezo wa uharibifu mkubwa kwenye nyota hiyo ya Rais wa Marekani ambapo imekuwa ikiharibiwa mara kadhaa kwa watu kuibomoa hadi kupelekea kuwekewa ulinzi mkali. Uharibifu wa safari hii umekuja kufuatia maandamano yanayoendelea nchini humo kupinga ukatili wa polisi dhidi ya jamii ya watu weusi.
No comments