Uingereza: Mume wa Malkia Elizabeth II, Mwanamfalme Philip atimiza miaka 99
Mwanamfalme Philip ambaye ni mume wa Malkia wa Uingereza, Elizabeth II kwa zaidi ya miongo 7 anasherehekea miaka yake 99 ya kuzaliwa, leo Juni 10
Philip 'The Duke of Edinburgh' atatumia muda wake katika nyumba ya Kifalme ya Windsor huko Magharibi mwa London ambapo yeye na Mkwe, Elizabeth (94) wapo kwa kipindi hiki cha 'lockdown'
Hiyo inamaanisha kuwa Wanafamilia wengine watatuma salamu za kumtakia heri ya kuzaliwa kwa kutumia mazungumzo ya video (video calls)
Mrithi wa Malkia Elizabeth ambaye pia ndio mtoto mkubwa kati ya watoto wanne wa Philip, Mwanamfalme Charles amesema hajamuona baba yake kwa muda mrefu sana
Philip alijitoa katika majukumu ya kifalme Agosti 2017 baada ya kukamilisha zaidi ya matukio 22,000 na hivi karibuni amekuwa akionekana mara chache hadharani ila Aprili 2020 alionekana alipotoa shukrani kwa wanaohusika na kupambana na #COVID19
No comments