Polisi Sita Kushtakiwa kwa mauaji Wakati wa Marufuku ya Kutembea Usiku Kenya
Polisi 6 watashtakiwa kwa makosa ya mauaji na unyanyasaji, kwa kuhusishwa katika matukio ya kufyatua risasi dhidi ya raia wakati wakihakikisha marufuku ya kutotembea usiku inatekelezwa
Ripoti ya mamlaka inayoangazia makosa ya Polisi nchini humo (IPOA) imesema, Wakenya 15 wameuawa na Polisi katika kipindi cha marufuku ya kutotembea usiku ili kudhibiti maambukizi ya CoronaVirus
Ripoti nyingine ya #HakiZaBinadamu ya Umoja wa Mataifa, imesema kuwa kulikuwa na ghasia za Polisi katika jamii zipatazo 182, vurugu hizo zilijumuisha kupiga watu, kurusha mabomu ya machozi, unyanyasaji wa kingono na kuharibu mali za watu
Kati ya watu waliouawa ni Yassin Moyo(13) aliyeuawa Machi 28. Yassin amedaiwa kupigwa risasi tumboni na Polisi siku moja baada ya marufuku ya kutembea usiku kuanza kutekelezwa
No comments