Header Ads

Header ADS

Nani Azifikishe Salamu Zangu Kwa Ali Kiba?


.
By SanguJoseph

Leo nataka tuwaze pamoja, Kwa nyinyi kupokea salamu zangu kwa Alikiba,, msianze kusema wewe Sangu J unachuki Zako binafsi na Kiba, mbona kila siku wewe unamuangalia kwenye kumkosoa na si kumpongeza jibu lako nitakwambia nafanya hivyo kwa sababu nahisi sehemu aliyopo Alikiba hastahili kuwepo kiufupi anajichelewesha mwenyewe, hivyo mnisaidie kumfikishia salamu zangu.

Tukiwa tunaendelea kuinjoy So Hot , tuanzie hapo kwenye kujichelewesha mwenyewe, wote tunajua Dunia imetoka kwenye Janga la Corona, lakini sijaona Project binafsi ya Alikiba (Achana na Post za Assas) akijenga awareness kwa wananchi kuhusiana na Corona, Kwa sababu tumeona Wasanii wenzake kama Rayvanny , Harmonize, Diamond, Darrasa, Snura wote walifanya mambo binafsi kama Wasanii kutengeneza Social awareness kuhusiana na Ugonjwa huu, lakini kwa mfalme aliishia kupost Awareness za Assas ambazo sio mbaya lakini nadhani kama Msanii alipaswa kuwa na Project yake peke yake.

Wakati wa Ugonjwa huu tuliona Rayvanny alitoa wimbo akimshirikisha Magufuli, Harmonize alitengeneza video ambayo ilichezwa vituo vingi, Diamond mpaka kaimba wimbo Quarantine.

Njoo hapa tena kwanini Kiba anajichelewesha sasa unaona wasanii wakiijiandaa na Kampeni, kwa kutunga nyimbo zinazohusiana na masuala ya siasa, tumeona Nandy, Beka Flavour, Harmonize, Petter Msechu, licha tu ya wimbo lakini baadhi ya Wasanii unaona kuna content wanazopost au kuzungumza wakijipanga kwa ajili ya kampeni.

Hapa mtasema Sangu unataka Alikiba ajiingize kwenye siasa, wakati yeye ni Msanii wa wote, Nitakujibu ndugu kampeni ni Opportunity ya kukutana na mashabiki na kuingiza Pesa kama ilivyo kwenye Fiesta, Wasafi Festival, Mziki Mnene Ali Kiba Tour na mkumbuke kama kampeni zitaenda kwa miezi 3 means kama Msanii akilipwa laki 1 (Si uhalisia nimekadiria tu) kwa show, Kwa miezi 3 una kama Mil. 9.

Sasa pima mwenyewe hivi wewe ndiyo unagombea nafasi Fulani na unataka kufanya kampeni unamfikiria kumpa nani nafasi akusaidie kuburudisha wananchi wako na katika kapu kuna Nandy, Harmonize, Diamond na Alikiba utamchukua Nani? ndiyo maana nasema anajichelewesha wenzake wamempita hatua 3 mbele, Ila muda haujaisha sana anaweza fanya chochote.


No comments

Powered by Blogger.