Hamisa Mobeto Amkataa Diamond Platnumz "Sitaki Kupoteza Muda"
“SITAKI kumzungumzia Diamond Platnumz!” Kauli hii imetolewa na mwanamitindo na msanii wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto ‘Misa’ juu ya baba wa mwanaye, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Kauli hiyo ya Misa aliyoitoa wikiendi iliyopita kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio nchini Uganda, imetafsiriwa kuwa, huko ni kumkataa jamaa huyo na huwenda hawana maelewano mazuri.
Mobeto na Diamond au Mondi waliwahi kuwa wapenzi kwa kuchepuka wakati jamaa huyo akiwa kwenye uhusiano ‘serious’ na mwanamama Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambapo walijaaliwa mtoto mmoja wa kiume aitwaye Dyllan aliyezaliwa Agosti 8, 2017.
Katika mahojiano hayo, Misa aliulizwa anajisikiaje kuwa mzazi mwenza wa Mondi ambaye ni staa mkubwa, ndipo akafunguka;
“Kiukweli sitaki kusikia au kupoteza muda wangu kumzungumzia Diamond kwa sababu alikuwa zamani na siyo mpenzi wangu kwa sasa.
“Siyo jambo ambalo ningependa kuzungumzia. Hayo yalishapita zamani,” alisema Misa ambaye ni Mkurugenzi wa Maduka ya Mobeto Styles Boutique.
Katika majibu yake, Mobeto alikwepa kabisa jambo lolote lililohusiana na Mondi kwa madai kwamba hataki kumzungumzia jamaa huyo.
Hata hivyo, alipoulizwa juu ya changamoto alizopitia alipokuwa kwenye uhusiano na Mondi alisema kuwa, uhusiano wowote una changamoto zake bila kujali ni wa staa au wa mtu wa kawaida.
“Kama umepangiwa wa kwako, utakuwa naye hadi mwisho wenu, lakini kama hujapangiwa, hautadumu iwe kwa staa au kwa yeyote,” alisema Misa.
Alipoulizwa aliwezaje kuendelea na maisha baada ya kuachana na Mondi, Misa alisema anamshukuru Mungu kwa sababu aliweza ku-move on (kusonga mbele) kwa haraka zaidi.
“Najua ni ngumu kwa mwanamke ku-move on kwa haraka, lakini kwa upande wangu haikuwa ngumu kwa sababu niliamini kwamba kama mtu umepangiwa wa kuwa naye, utadumu naye, lakini kama hujapangiwa huwezi kudumu naye. “Kila kitu hutokea kwa sababu fulani, kwa hiyo kama uhusiano ukikukataa, huwezi kulazimisha au kufanya chochote ili udumu ndani yake. “Njia pekee unayoweza kupita ni ku-move on,” alisema Misa ambaye mbali na kufanya muziki, pia ni mbunifu wa mavazi, mwigizaji na mfanyabiashara.
Misa alitaka kuulizwa zaidi kuhusu ubunifu na biashara ya nguo ambapo alisema yupo mbioni kufungua matawi ya maduka yake ya nguo nchini Uganda.
“Nipo mbioni, natafuta mawakala wa maduka yangu ya Mobeto Styles Uganda,” alimalizia Misa ambaye anafanya vizuri na wimbo wake wa Sensema aliomshirikisha Whozu.
No comments