Msamaha wa Magufuli kwa zimamoto watoka na onyo kali
Rais Magufuli amesema amemsamehe aliyekuwa Kamishna wa Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye baada ya kumuomba msamaha kwa zaidi ya mara tatu na viongozi wengine katika jeshi hilo ambao ilitakiwa awafukuze.
Amesema kwa upande wa Andengenye, hawezi kumrudisha katika Jeshi hilo ila ataonekana katika kazi nyingine kwani mtu akiomba msamaha na kuonesha kutubu inabidi asamehewe
Rais Magufuli ametangaza msamaha huo huku akitoa onyo kwa askari wa Jeshi la Zimamoto juu ya uchukuaji wa rushwa na kuingia mikataba isiyo na tija kuacha mara moja ambapo amewaambia kuwa fedha za bure katika kipindi chake ni mbaya zitawaharibia maisha yao.
Amesemahayo leo Juni 11 2020, alipokuwa anazindua jengo la makao makuu ya jeshi hilo mjini Dodoma huku akiwasifia kuwa jeshi hilo ni sawa na malaika wa duniani hivyo hawapaswi kufanya mambo mabaya kwa kuanzisha moto.
JPM ‘awajibu’ wanaopanga kumuongezea muhula wa tatu madarakani
“Fedha za bure kwenye kipindi changu ni mbaya zitawaharibia maisha na mimi hata ukaloge namna gani sibadiliki ninachokitaka fedha za walipakodi zikawaletee mabadiliko” amesema Rais Magufuli
Ikumbukwe kuwa mapema January 23 2020, Rais John magufuli alitengua uteuzi wa aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Kangi Lugola na Andengenye kutokana na kuingia mkataba mbovu uliolengwa kusaidia jeshi la hilo.
No comments