Header Ads

Header ADS

Lord Eyes avunja ukimya kwa Ray C kuhusu madawa

 
Mkali wa HipHop kutokea Kaskazini mwa nchi ya Tanzania yaani Arusha Lord Eyes, amefunguka na kusema hajawahi kumfundisha aliyekuwa mpenzi wake Ray C kutumia madawa ya kulevya bali alimkuta tayari kashatumia.

Lord Eyes amesema hayo kupitia show ya SalamaNa ya East Africa TV ambayo inaruka kila siku ya Alhamisi kuanzia 3:00 usiku, wakati anajibu madai ya kumfundisha Ray C kutumia madawa ya kulevya walipokuwa kwenye mahusiano.

"Nimekutana na Ray C tayari alikuwa ameshawahi kutumia japo mimi nilimficha, nikiwa naye situmii ila nikiwa na kampani yangu natumia, sasa hadi ile kampani yangu ikamfikia, sijawahi kumfundisha mtu, hata mimi nilikuwa sijui nilipewa nikaonja, Madawa ya kulevya ni kama shetani anavyokuingia, familia yangu ikawa inalia sana kama hujawahi kuonja usiguse hiyo kitu kiukweli" ameeleza Lord Eyes

Aidha ameongeza kusema "Nilimpenda sana Ray C, hadi ilifika level ambayo nikawa namuogopa ila ana upendo na ni mzuri sana, wivu ndiyo ulipelekea sisi kuvurugika, sasa hivi huwa tunawasiliana mara moja moja ila namkubali".


No comments

Powered by Blogger.