Mdee na Bulaya watua Takukuru
Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee na Mbunge wa Bunda Mjini (Chadema), Ester Bulaya wamefika katika ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa.
Mdee na Bulaya wameingia katika ofisi hiyo majira ya saa 05:00 asubuhi wakiwa wamevalia barakoa kwaajili ya kuhojiwa juu ya Tuhuma zinazo kabili Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.
Wabunge hao wanahojiwa kuhusiana na matumizi mabaya ya fedha za Chadema ambazo zimelalamikiwa na wabunge waliotoka katika chama hicho
No comments