Header Ads

Header ADS

Lil Wayne Apata Mpenzi Mpya Baada ya Kuachana na Mrembo La'Tecia Thomas


Baada ya kuachana na mrembo La'Tecia Thomas, Lil Wayne anaonekana anapenda sana wasichana wanamitindo, ametajwa kutoka kimapenzi na mwanadada mrembo mwenye asili ya Puerto Rico-Kuwait aitwaye Denise Bidot.

Uvumi wa wawili hawa kuwa kwenye mahusiano ulianza pale ambapo Wayne alionekana kum-follow mrembo huyo pekee kwenye instagram. Pia juzi Ijumaa (June 12) wakati akipiga stori na Nicki Minaj kwenye Young Money Radio, alimwambia kuwa sasa ana mpenzi mpya kwenye maisha yake.

Denise ni mwanamitindo ambaye amefanya kazi na makampuni mbali mbali kama Savage x Fenty, Lane Bryant na Levi's. Pia amepita kwenye majukwaa makubwa ya maonesho ya mitindo kama New York Fashion Week

No comments

Powered by Blogger.