Header Ads

Header ADS

Dokta Mwaka Agusia Kuongeza MKE Namba Nne...."Naoa Kwa Sababu ya Tamaa tu"


Daktari wa tiba asilia, matatizo ya afya na uzazi kwa wanawake Dkt Mwaka, ameeleza kuwa sababu ya kuoa wake watatu ni tamaa tu, na kwamba hata mke wa pili na watatu amewaoa bila kuangalia vigezo vyovyote.

Dkt Mwaka amesema hilo kwenye kipindi cha MamaMia ya East Africa Radio, wakati anaeleza sababu ya kuoa wake watatu na mpango wa kuongeza mke wa nne. "Sijawahi kuangalia vigezo vyovyote mara nyingi wanaume huwa tunaoa kwa sababu ya tamaa, unaweza ukamuona binti ukavutiwa naye kama hupendi udhinifu ndiyo unaoa, ila kiukweli kinachokusukuma hapo mwanzo ni matamanio tu, mke wangu wa pili na watatu sikutazama vigezo lakini nashukuru Mungu naishi nao vizuri mpaka leo" ameeleza.

Aidha Dkt Mwaka ameongeza kusema "Wanaume wote wanatamaa ila kinachotokea ni kujizuia tu kwa sababu mbalimbali, hata nikifikisha wake wanne haina maana kama tamaa itaisha lakini kisheria nitakuwa nimefikisha kiwango cha kutosheka nacho".


No comments

Powered by Blogger.