JPM Awaonya Askari “Fedha Za Bure Zitawaharibia”
COVID-19: John Magufuli declares Tanzania free of the pandemic - CGTNRais John Magufuli amewaonya askari wa jeshi la zimamoto juu ya uchukuaji wa rushwa na kuingia mikataba ya kibepari kuacha mara moja kwan rushwa kwenye kipindi chake zitaharibu kazi na maisha ya kazi.
Akizungumza leo Juni 11 2020, alipokuwa anazindua jengo la makao makuu ya jeshi la hilo mjini Dodoma amesema jeshi hilo ni sawa na malaika wa duniani hivyo hawapaswi kufanya mambo mabaya kwa kuanzisha moto.
“Jamani pesa za bure kwenye kipindi changu hiki ziacheni, zitawaharibia maisha yenu bure na ubaya mimi hata ukaloge namna gani sibadiliki ninachokitaka ni mabadiliko ya wananchi alafu nyinyi ni kama malaika wa dunia kwakua mnazima moto ambao una hathiri watu” amesema.
Ikumbukwe kuwa mapema January 23 2020, rais John magufuli alitengua uteuzi wa aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Kangi Lugola kutokana na kuingia mkataba mbovu uliolengwa kusaidia jeshi la hilo.
No comments