HISTORIA Fupi ya Mwanamapinduzi CHE GUEVARA, Alivyokamatwa na Kuuawa KIKATILI Kama Mnyama
Jina kamili : Ernesto Guevara
Kazi : Daktari, mwanamapinduzi wa kijamaa (marxist)
Uraia : Argentina
Kuzaliwa : June 14 1928
Kufariki : October 9, 1967 ,Bolivia milima ya La heguera
Chanzo cha kifo : kuuwawa kwa kupigwa risasi
Kama kijana msomi wa shahada ya udaktari, che Guevara alisafiri nchi nyingi sana huko bara la Amerika ya kusini na rafiki yake, akawa ni mtu mwenye uchungu mkubwa kuona maisha ya dhiki,njaa, magonjwa nchi za America ya kusini, akawa na mwamko mkubwa kubadili hali ile kwa kuwa aliamini ya kuwa mfumo wa ubepari ndio chanzo kikubwa kilichokuwa kinaitafuna Latin America.
Miaka ya 50 akiwa anasoma udaktari huko Mexico Che Guevara alikutana na Fidel Castro na Raul Castro ambapo watatu hao walipanga mapinduzi ya kumg’oa raisi wa Cuba wakati huo Fulgencio batista ambaye alikuwa na huhusiano wa kimaslahi na America, Che akapata nguvu na uaminifu mkubwa kutoka kwa Fedel Castro na kupandishwa kuwa kiongozi wa wanamgambo (guerilla insurgents)
Punde tu baada ya Fulgencio batista kukimbia CUBA,Che alihusika kama mtu muhimu katika serikali ya Cuba iliyoongozwa na Fidel Castro, akiwa kama Gavana wa benki kuu ya Cuba ambapo saini yake ilianza kutumika katika noti za CUBA , baadae kama waziri wa kilimo wa Cuba.
Mwaka 1964 akiwa kama mmoja ya msafara wa watu wa serikali ya Cuba umoja wa Mataifa New York MArekani, aliweza kupata “sifa” ya “mwanamapinduzi halisi wa kukumbukwa” pale alipotoa hotuba ndefu katika ukumbi wa UN akilaumu wazi ukimya wa Umoja huo juu ya kilichokuwa kinaendelea Afrika ya kusini (ubaguzi wa Rangi) alinukuliwa akisema
“wale wanaoua watoto wao na kuwabagua kila siku kwa sababu ya rangi ya ngozi zao, wazungu wanawaua watu weusi na hawakamatwi, serikali ya kikaburu inawalinda wauaji, na mbaya Zaidi inawaadhibu watu weusi kwa kuwa tu wanatataka haki zao na utu wao, vipi watu hawa (makaburu) wakaitwa watetezi na walinzi wa Amani?”
MGOGORO WA CONGO – DRC
Miezi michache baada ya kutoa hotuba UN, Che alitoweka katika maisha ya kawaida “public life” na hakuna aliyejua alikwenda wapi mpaka baadae ilipokuja gundulika Che alikuwa akipigana sambamba na Laurent Kabila huko Congo dhidi ya wabeligiji na baadhi ya wapiganaji wa ki cuba waliokuwa Afrika, vita ambayo ilishindikana na akakimbilia Tanzania na kukaa maeneo ya karibu na ziwa Tanganyika na baadae Dar es salaam huku akiishi kwa kujificha
Baadae mwaka 1966 alirejea Cuba kumuaga kwa Fudel castro na kusafiri kwenda Bolivia kuendeleza harakati zake za kuzikomboa nchi za America ya kusini kutoka kwenye makucha ya Ubepari…aliingia Bolivia akiwa kama mfanyabiashara hasiyejulikana baada ya kunyoa upara, kuweka mvi bandia na kuyoa ndevu zake zote, akaweka kambi na baadhi ya wapiganaji wenzake aliowakuta Bolivia maeneo ya milima ya montane dry fores
KUKAMTWA NA KUUWAWA
Mwaka 1967, makachero wa Bolivia wakisaidiwa na CIA amabye alikuwa akiwakilsha ndugu Felix Rodriguez waligundua maficho ya ache na kundi lake huko milimani Bolivia, asubuhi ya October 8 mwaka 1967 wanajeshi takribani 1,800 walizingira maeneo yoote ya milima walikokuwa wamejificha akina Che na ikapiganwa vita ya masaa kadhaa na Che akipigwa Risasi za miguu na kukamatwa na wenzake,
Yasemekana baada ya kuzidiwa katika mapigano yale alisema
“Usifyatue risasi, mi ni Che Guevara nina thamani kubwa kuwa hai kuliko kunikamata nimekufa”
Alifungwa kama na wenzake akakamatwa na kupelekwa kijiji cha La higuera ambapo baada ya raisi wa Bolivia ndugu kusikia amekamtwa alitoa amri auwawe haraka sana, wakati huo huo CIA walimtaka apelekwe Panama akahojiwe kwa kina na salama yake ili hasiuwawe alikuwa apelekwe America japo haikutokea.
Siku moja kabal ya kuuwawa alichukuliwa na baadhi ya wanajeshi na kupiga picha ya kumbukumbu na kesho yake akauliwa na askari mmoja aliyejitolea na kumpiga risasi sita za kifua na kufa palepale
Kabla hajapigwa risasi na muuaji wake haya ndio yalikuwa maneno yake ya mwisho
“Najua umekuja kuniua, shoot mtu mwoga wewe!!! na ufahamu utakua umeua mwanaume kamili”
Aliacha wake wawili na watoto watano
No comments