Rais Magufuli: Tusidharau dawa za kienyeji, mchawi tu ndio mbaya
Rais John Magufuli amesema hakuna haja ya kudharau dawa za kienyeji kwa kuwa miti yote imeumbwa na Mungu kwa ajili ya binadamu.
“Tunamshukuru Mungu kwa kutuepusha na ugonjwa wa Corona mambo yanakwenda vizuri tusidharau dawa za kienyeji, tusidharau hata kidogo mchawi tu ndio mbaya lakini miti yote iliumbwa na Mungu kwa ajili ya kutusaidia sisi,” amesema Rais.
Rais amesema ameshatoa maelekezo kwenye wizara ya afya kile kitengo cha dawa asilia kiendelezwe kwa nguvu zote na bajeti yake iongozwe.
“Ili watu wanavyotengeneza madawa yao tusiwadharau kumekuwa na katabia cha watu wanaotengeneza dawa za kienyeji wanasemwa madawa yamepitwa na wakati wewe ndio umepitwa na wakati. Madawa ya kienyeji ni tiba kama ilivyo madawa mengine tulipumbazwa kuwa tusiamini tulicho chetu tuamini kilicho chao,” alisema
Rais amewaomba vitengo vyote vinavyoshughulikia dawa za asili na wale wote wanaofanya kazi halali kwa kutumia dawa za asili wasaidiwe.
“Ndio maana ukienda katika nchi zilizoendelea hata China kuna dawa na pia kuna dawa za asili na yapo maduka kabisa hata Ulaya, hata Canada kuna maduka ya dawa za asili. Niwaombe Watanzania na wizara husika tusidhara vya kwetu tuviendeleze ili tuweze kupambana na magonjwa mbalimbali,,” amesema Rais.
No comments