Header Ads

Header ADS

Je, Unafahamu Chuo Kikuu cha Kwanza Duniani Kilijengwa Afrika?

Timbuktu ulikuwa mji mashuhuri duniani enzi hizo za karne nyingi zilizopita, mji huu ulikuwa ndiyo mji mkuu wa nchi ya Mali; si rahisi leo hii kwa mtu yeyote kuamini kwamba chuo kikuu cha kwanza duniani kilijengwa nchini Mali hasa kwa vile nchi hiyo ya Mali hivi sasa ni nchi ambayo imerudi nyuma sana kimaendeleo si kidunia tu bali hata kwa kiwango cha nchi za Kiafrika! Zaidi ya miaka elfu elfu mbili iliyopita Mali iliweza kujenga utawala madhubuti wa kifalme ambao ulivuma Afrika nzima na hata duniani kote, hasa pale ambapo raia wake wenye ujasiri mkubwa Mandingos waliweza kusafiri kila kona ya dunia wakitafuta biashara na utafiti wa aina mbalimbali!



Wakati wa utawala huo wa kifalme wa kabila la Mandingos ulipokuwa unavuma ndipo walipoweza kujenga chuo kikuu cha kwanza duniani, ambacho kilifanya tafiti mbalimbali za kisayansi na kufundisha vijana wengi waliotoka nchini Mali na nchi za jirani. Wakati huo nchi za ulaya bado hazijaamka zipo nyuma sana, tukumbuke maendeleo ya wazungu yameanzia Ugiriki na Hispania ambayo yameanza kwenye millennium ya pili wakati hii tuliyokuwa nayo sasa ni ya tatu; vyuo vikuu vya ulaya vya mwanzo vilianza kujengwa karne ya 16 wakati huo utawala wa kifalme wa Mandingos umeshavuma karne nyingi zilizopita na umeshaanza kusambaratika.

Watu wa nchini Mali au kwa jina mashuhuri hujulikana kama Mandingos ndiyo watu wa kwanza duniani kuanza kufanya hesabu wakati wa 35000 BC na mahesabu waliyokuwa wakiyafanya yalikuwa ya kuhesabu mifupa ya binadamu na wanyama; wakati huo wazungu wapo nyuma sana, na baada ya waafrika kugundua mahesabu wakafuatiwa na waarabu, na baada ya waarabu wakafuata wahindi na wachina, na mwishowe ndiyo wazungu wakaanza nao kufanya hesabu na kuziendeleza hadi leo.

Mandingos walikuwa ndiyo watu wa kwanza duniani kuanza kumfanyia binadamu operation na kumshona kwa kutumia nyuzi za mishipa ya ndama wa ng’ombe mdogo; Mandingozi walikuwa pia ndiyo watu wa kwanza duniani kuwa tekinolojia ya kuchimba dhahabu na kutengeneza vito mbalimbali vinavyotokana na dhahabu.

Michoro ya majengo unayoikuta leo hii kutoka kwenye majengo ya ulaya kama vile Spain, Italy, Greece, France, na Uarabuni yote iliigwa kutoka Timbuktu – Mali miaka hiyo ya nyuma na kuboreshwa na waigaji kutoka ulaya na uarabuni.

Kuna wazungu ambao wanakubali ukweli kwamba Timbuktu ndicho chuo kikuu cha kwanza duniani, hasa wakizingatia kwamba kuna mwanahistoria mmoja kutoka Ufaransa ambaye alishawahi kuandika kitabu chake kuhusu ukweli wa historia ya dunia, lakini kitabu hicho wazungu walikipiga vita na kununuliwa chote sokoni na hakijawahi kuchapishwa tena, niliwahi kukisoma kitabu hicho ila nilijisahau sikuchukuwa jina kamili la mwandishi wa kitabu hicho, lakini mwenye nakala ya kitabu hiki adimu ni rafiki yangu kutoka nchini Benin – West Africa ambaye anaishi uhamishoni nchini Canada kwenye jimbo la Quebec.

Kanungila Karim

No comments

Powered by Blogger.