Header Ads

Header ADS

Uchebe Amtaka Shishi Akate Tumbo



ZUWENA Moha-mmed almaarufu Shilole au Shishi Baby ni mwanamama Bongo Fleva amekiri kuwa mumewe, Ashraf Uchebe amemtaka kukata tumbo kutokana na kuwa mnene sana.

 

Shishi ambaye pia ni mjasiriamali wa kuuza chakula, ameiambia OVER ZE WEEKEND kuwa, mara nyingi Uchebe amekuwa akimsifia na kumwambia anazidi kuwa mzuri licha ya kuwa nje watu wanakesha kumwambia apungue, jambo ambalo haliafiki sana zaidi ya kumwambia apunguze tu tumbo.

 

“Nafanya sana mazoezi ya kupungua, lakini unene wangu siyo kero kwa mume wangu, tena ndiyo anazidi kunipenda. Mara nyingi ananiambia mwili wangu mzuri ila nijitahidi kupunguza tumbo tu,” anasema Shishi anayekimbiza na ngoma yake mpya ya Pindua Meza.




No comments

Powered by Blogger.