Trump Amjibu Powell “Ulikuwa Dhaifu Sana Kwenye uongozi wako”
Rais Trump alijibu kwa kumtaja Powell kuwa mtu aliyepewa “hadhi ya juu kuliko anavyostahili”.
Katika mtandao wake wa Twitter, Bwana Trump alisema Colin Powell ni “mtu ambaye alitakiwa kuwajibika sana kwa kutupeleka kwenye Vita vya Mashariki ya Kati”, akiashiria vita vya Ghuba vya mwaka 1990-93 na hatua ya Marekani kuvamia kijeshi Iraq mwaka 2003.Bwana Biden pia alitumia Twitter yake kumkosoa Trump kwa jinsi alivyoshughulikia maandamano, na kusema kuwa “ametumia visivyo [maneno kama Rais] kuchochea vurugu, kuleta chuki na mgawanyiko, ana kututenganisha zaidi”.
Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani Condoleeza Rice ameiambia CBC New kwamba angelipendelea Trump ”aachane kidogo na Twitter” na kufanya mashauriano na Wamarekani.
“Sio kila mtu atakubaliana na Rais, lakini kwa hili, Rais huna budi kusema na kila Mmarekani, na wala sio wale tu wanaokubaliana na wewe,” alisema.
No comments