Wema Sepetu Adai Kuna Watu Wake wa Karibu Wanamrudisha Nyuma
Nyota wa Bongo Movie Wema Sepetu ametumia ukurasa wake katika mtandao wa instagramu kueleza kuwa kuna watu wake wa karibu kumrudisha nyuma lakini bado anaenenda vyema hata hivyo amekuja kugundua kuwa wakati mwingine anajilaumu yeye kimakosa.
Wema amesema “Kuna wakati mtu unaweza kujiuliza wapi unakosea na ukajilaumu sana kwa makosa ambayo hata wewe mwenyewe huwezi kuelewa… Nimekuwa nikipitia sana hali hii, na nimekuja kugundua kwamba kumbe kuna watu ambao sometimes wanaweza kuwa ni watu wako wa karibu sana wapo tu wanasubiria kuku outshine pale wanapoona unashine.
“Unachopaswa kufanya ni kusonga mbele na kutoangalia nyuma… Huwa inakua ngumu sana at times maana design wanakurudisha nyuma kimtindo but dont lose Hope… Keep Going kwa maana naamini kama Mungu kakuandikia Ipo basi Ipo tu”.
A Lil Monday Motivation To Never lose Hope my Loves… Inanihusu pia Saaaaana hii… (Sadly😔) .
No comments