Header Ads

Header ADS

Vigogo wa Chadema Wampopoa Mbunge wao Aliyeomba Kuhamia CCM kwa Machozi


Mbunge Lijualikali aangua kilio Bungeni, amponda vikali Mbowe na ...Viongozi mbalimbali wa Chama cha Chadema wamemshambulia Mbunge wa Kilombero Peter Lijualikali kutokana na hatua yake ya kutangaza kuomba kujiunga na CCM leo huku akibugujikwa na machozi na kusema yupo tayari kufanya kazi yoyote ile ila sio kuendelea kuwa chadema.

Akiongea leo Bungeni Lijualikali amesema anaomba kujiunga na CCM pale muda wake wa ubunge utakapokwisha akisema amechoka kuendelea kutumika vibaya ndani ya chama chake cha sasa.

Lijualikali alizungumzia misukosuko yake ndani ya chama hicho dhidi ya dola na suala la chama chake kumkata posho kwa ajili ya ujenzi wa Chama.

Hata hivyo viongozi wa Chadema katika yote wameshikilia suala la posho wakisema lipo kwa mujibu wa Sheria lakini pia wamechombeza kuwa kura za maoni ndani ya chama hazijamkalia vizuri.

Lijualikali ni miongoni mwa wabunge wa Chadema waliotakiwa kujieleza kwa chama kwanini walikiuaka maelekezo ya mwenyekiti wa Chama kwa kuingia Bungeni hata hivyo wenzake wanne walifukuzwa uanachama.




No comments

Powered by Blogger.