Waziri Kigwangalla Asema Wamiliki wa Hoteli Kutenga vyumba kwa Ajili ya Kupiga Nyungu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla, amesema wanawashawishi waendeshaji wa utalii na wamiliki wa hoteli kutenga vyumba maalum kwa ajili ya kupiga nyungu .
“Wamiliki wa hoteli kutenga vyunba maalum kwenye Spa zao kwa ajili ya kupigia nyungu ya mitishamba, marashi na miti dawa yetu ya asili,” aliandika Kigwangalla katika ukurasa wake wa Twitter.
Kigwangalla amesema tiba asilia imesaidia sana kwenye ugonjwa wa Corona .
“Hatutaki kusema tu lakini kiukweli tiba asili imerusaidia sana kwenye Corona ! Tuiuze nje sasa
Tunawashawishi waendeshaji wa utalii na wamiliki wa hotel kutenga vyumba maalum kwenye Spa zao kwa ajili ya kupigia ‘nyungu’ ya mitishamba, marashi na miti dawa yetu ya asili. Hatutaki kusema tu lakini kiukweli tiba asili imetusaidia sana kwenye Corona! Tuiuze nje sasa! pic.twitter.com/w4LWEkyMyK— Dr. Kigwangalla, H. (@HKigwangalla) May 18, 2020
No comments