Sukari Yawa Shubiri Kwa Wafanya Biashara...Wanane Wakamatwa Kwa Kukiuka Agizo la Serikali
Wafanyabiashara 8 wa Sukari, mkoani Mtwara wamekamatwa kwa kukiuka agizo la Serikali kuhusiana na uuzaji wa kuuza Sukari kinyume na bei elekezi ya iliyotolewa.
Agizo la kukamatwa wafanyabiashara hao limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelesius Bakanwa, ambapo amefkia uamuzi huo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi.
"Nimefanya uchunguzi tumebaini karibia Wilaya zote hakuna mfanyabiashara aliyetii agizo la kuuza sukari kwa bei elekezi, ni Tandahimba pekee ambapo baadhi ya wafanyabiashara wametii" amesema RC Bakanwa
"Mpaka jana tumewakamata wafanyabiashara nane, na tumekamata kilo za Sukari 431" ameongeza Mkuu wa Mkoa Bakanwa
No comments