Roketi Laanguka Karibu na Ubalozi wa Marekani, Baghdad
Kumetokea shambulizi la roketi karibu na ubalozi wa Marekani ulioko mjini Baghdad mapema leo, likiwa ni la kwanza kuanguka kwenye eneo hilo lenye ulinzi mkali.
Duru za usalama zimeliarifu shirika la habari la AFP. Mripuko wa roketi hiyo huenda ulisikika kote mjini humo na kusababisha ving'ora vya usalama kulia kwenye ubalozi huo, ingawa hata hivyo haukusababisha madhara yoyote.
Hakukua na taarifa ya haraka ya wahusika wa shambulizi hilo. Shambulizi hilo la roketi linafuatia mashambulizi kadhaa kama hayo dhidi ya maslahi ya Marekani nchini Iraq tangu mwezi Oktoba, ambayo Marekani iliyalaumu makundi yanaoungwa mkono na Iran yaliyoko miongoni mwa vikosi vya usalama vya nchini humo.
Mashambulizi hayo yaliyosababisha vifo vya watumishi raia wa Marekani, Uingereza na Iraq kwa kiasi kikubwa yametia doa mahusiano kati ya Baghdad na Washington.
No comments