Serikali Yatangaza Utaratibu Mpya Kwa Watalii “Hawarudi Nyumbani Mwezi Mmoja”
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, ametangaza kufunguliwa kwa anga la Ndege la Tanzania, ambapo kwa sasa Ndege za Kitalii, na kibiashara zitaruhusiwa kuingia nchini.
Aidha ameitaka ATCL kujipanga ili kurejesha huduma za usafiri.
Wakati huohuo akizungumza Jijini Dodoma, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamis Kigwangalla amesema kuanzia sasa watalii wanaruhusiwa kuingia nchini na kupimwa.
Dr. Kigwangalla amesema katika zoezi hilo wahudumu wa Viwanja vya Ndege, pamoja na wahudumu wa watalii watalazimika kupimwa Corona kila mara pindi wanapoingia Tanzania.
Aidha Waziri Kigwangalla amesema, Wizara ya Uchukuzi kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, zitasimamia miongozo maalumu iliyowekwa ikiwamo kufungua anga ili kuruhusu ndege zianze kuingia.
No comments