Header Ads

Header ADS

Mahakama Yamtaka Rick Ross Kutoa Matunzo ya Mtoto



Rapa Roozey Rich Forever, ametakiwa na Mahakama kutoa pesa kwa ajili ya matunzo ya watoto wake wawili aliozaa na ex-girlfriend wake Briana Camille .
.
Kwa mujibu wa nakala za mahakamani zilizochapishwa na mtandao wa BOSSIP , vithibitisho vyote ikiwepo Vipimo vya DNA vinaonyesha kua Rozzey ndio baba wa watoto hao, hivyo hana namna zaidi ya Kuchukua majukumu ya kuwahudumia . .
.
Rozzey na Briana walikua wapenzi kwa muda mrefu, kabla ya kuhitalifiana na Rozzey kuamua kumfukuza kwenye Jumba lake akiwa na watoto wawili , na kwa Mujibu wa Briana , Rozzey hajatuma pesa yoyote tangu mwezi February mwaka huu.

Wawili hao walikua na kesi juu ya matunzo ya watoto mahakamani, ambapo moja ya vithibitisho vilivyokua vinasubiriwa ni kipimo Cha DNA ambacho tayari kimethibitisha kua Rozzey ndio baba wa watoto hao .

No comments

Powered by Blogger.