Diamond, Nandy Jukwaa Moja na Idris Elba mei 25
Nyota wa muziki nchini, Diamond Platnumz na Nandy wamejumuishwa kwenye orodha ya wasanii wengine wakubwa Afrika katika tamasha la kuchangisha fedha ili kusaidia waathirika wa corona.
Alex Okosi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji anayehusika na YouTube, amesema tamasha hilo linaloitwa Africa Day Benefit Concert litafanyika Mei 25, mwaka huu na kuruka mubashara MTV Base huku mwigizaji wa Uingereza, Idris Elba akisherehesha tukio zima.
Mbali na wasanii hao kutoka Bongo, mastaa wengine watakaoshiriki tamasha hilo ni Sho Madjozi, AKA, Burna Boy, Sauti Sol, Yemi Alade, Teni,Toofan, Bebe Cool, Tiwa Savage, Stone Boy, Rema, Fally Ipupa na wengine kibao.
No comments