Header Ads

Header ADS

Kumekucha Huko...Balozi wa KENYA Aibuka...Rais Kenyatta Amenituma, Kenya Haiingilii Tanzania Adui Yetu ni Corona"

Rais Kenyatta amenituma hapa, anasema Kenya haiiangalii Tanzania kama jirani bali kama Ndugu, sisi sio maadui, adui yetu ni corona, ndio maana alikuwa Rais wa kwanza kuingia Chato kumsalimia JPM, akachukua dhahabu akasema mpelekeeni Magufuli” -Dany Kazungu, Balozi wa Kenya nchini Tanzania

“Bila hii corona April 26 mwaka huu Kenyatta alipanga aje asherehekee na Watanzania Muungano, alipanga awe na ziara ya muda mrefu hapa TZ kuliko Rais yeyote, uamuzi ambao Kenya imechukua kuhusu safari za mipakani sio kwasababu ya Tanzania bali adui yetu ni kirusi”-Balozi Kazungu

“Hakuna Mkenya anayemuombea mabaya Mtanzania, Wakenya tunawaombea Watanzania mpigane na janga hili, na sisi pia mtuombee, tusianze kukorogwa na kirusi hiki, tusianze kugongana kisa corona, Watu watulie, Viongozi wetu watakutana na tutalimaliza” -Balozi Kazungu

No comments

Powered by Blogger.