Profesa Tibaijuka Ampongeza Rais Magufuli Asema Tiba za Asili si Uchawi ni Sayansi
Mbunge wa CCM jimbo la Muleba Kusini Anna Thibaijuka amesema Rais John Magufuli amewapa nguvu watu wanaoamini katika dawa za asili huku akisema dawa asili si uchawi ni sayansi.
Hivi karibuni Rais John Magufuli akiongea na wakuu wa vyombo vya ulinzi kuhusu Mlipuko wa ugonjwa wa corona Covid-19 alisema ni wakati sahihi wa watu kuanza kutumia tiba za asili ikiwemo kujifukiza ili kupambana na ugonjwa huo.
“Kwa hili namshukuru Rais Dr. John Pombe Magufuli kutambua tiba za asili kwenye vita hii ya Corona, dawa za asili si uchawi ila ni sayansi,” amesema Tibaijuka.
Amesema kwa hatua hiyo ya Mugufuli amefanya jambo jema na sayansi hiyo itasaidia wazee na watoto na wanaobeza watambue kuwa hiyo ni elimu ya kwaida sio ramli.
No comments