Marekani yasisitiza kuwa Virusi vya Corona vinaogopa Miale ya Jua Hivyo Fainali Kiangazi
Mwanasayansi mmoja nchini Marekani leo Aprili 24 ameeleza kuwa virusi vya corona vinaharibiwa kiurahisi na na miale ya jua hivyo kuna matumani makubwa ya ugonjwa huo (Covid-19) unaoitesa dunai ukaisha wakati wa kiangazi.
hata hivyo tayari Shirika la Afya Duniani WHO lilisema mwanzoni mwa mwezi Aprili kwamba kukaa juani ama katika sehemu zenye joto jingi la zaidi ya nyuzi 25 hakuzuii kupata maambukizi ya virusi vya corona.
Mwanasayansi mwandamizi katika taifa la Marekani William Bryan ambaye ni mshauri wa masuala ya afya katika Serikali ya Bwana Donald Trump amewaeleza waandishi wa habari kulingana na utafiti uliofanyika huenda maambukizi ya corona yakapungua au kukoma wakati wa kiangazi.
“Utafiti wetu wa kuvia sana ni kuwa miale ya jua inaonekana kuua virusi vya corona waliopo mahali na waliopo hewani, kuongezeka kwa joto na unyevunyevu vyote vimekuwa na athari mbaya kwa ukuaji wa virusi vya corona,” amesema Bryan wakati akizungumza katika ikulu ya Marekani.
Hata hivyo utafiti huo haujawekwa kwa umma ili kuruhusu watalaamu huru nao kutoa mawazo yao lakini duru za sayansi zinaeleza kuwa kuna uhusiano mkubwa wa virusi hivyo kuuliwa na mionzi lakini hakuna uthibitisho kama mionzi iliyotumika ni sawa na ile inatokana na jua wakati wa kiangazi
No comments