Corona yabadirika utaratibu makanisani
Misa za Jumapili sehemu kubwa duniani hazitakuwa rahisi, kwa kuwa taratibu nyingi za kiimani huhusisha mambo yanayochukuliwa kuwa yanajenga mazingira ya kusambaa kwa homa ya virusi vipya vya corona vilivyopewa jina la Covid-19.
Nchini Italia, ambako wananchi wengi ni waumini wa Kanisa Katoliki, tayari watu 197 wamefariki kutokana na ugonjwa huo, jambo lililosababisha kufutwa kwa misa katika eneo kubwa la Kaskazini ya jiji la Roma kwa lengo la kuzuia kuendelea kusambaa kwa ugonjwa huo.
Jana Vatican ilisema kiongozi wa kanisa hilo duniani, Papa Francis ataendesha misa ya leo kwa njia ya mtandao katika jitihada za kukabiliana na ugonjwa huo ambao umeshaua watu 197 nchini Italia huku kukiwa na maambukizi 4,600 barani Ulaya.
Hiyo ni baada ya watu 49 kupoteza maisha ndani ya saa 24 nchini Italia.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 83 analazimika kuachana na utamaduni wa karne kadhaa kwa kutumia teknolojia kufanya maombi ili kuzuia maelfu ya watu kumiminika katika eneo la Kanisa la St. Peters Square kwa sala ya kawaida ya Angelus.
“Maombi yatarushwa moja kwa moja na Vatican News na katika runinga kwenye Uwanja wa Saint Peter’s,” Vatican ilisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
No comments