Watu 10 wafariki China kufuatia kuporomoka kwa Hoteli
Idadi ya watu waliopoteza maisha baada ya kuporomoka kwa hoteli moja iliyokuwa ikitumiwa kuwaweka watu chini ya karantini kutokana na virusi vya corona katika mji wa Quanzhou nchini China, imefikia watu 10.
Mamlaka nchini humo zimesema watu wengine 28 bado wamekwama kutokana na ajali hiyo. Awali zaidi ya watu 70 waliaminika kukwama katika jengo hilo la ghorofa saba lililoporomoka jana jioni.
Wakati wa mkutano na wanahabari uliondaliwa na serikali katika eneo la Quanzhou, maafisa wa serikali, wamesema kuwa kikosi cha uokoaji cha zaidi ya watu elfu moja ikiwa ni pamoja na maafisa wa zima moto, vikosi vya polisi pamoja na wahisani wengine, walifika katika eneo hilo jana usiku huku watu 43 wakiokolewa na 36 kati yao waliokuwa na hali mbaya walipelekwa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu
Shirika la habari nchini humo Xinhua, limeripoti kuwa ghorofa ya kwanza ya jengo hilo ilikuwa chini ya ukarabati wakati wa tukio hilo.
No comments