CCM watua mahakamani kulipa milioni 30 kumnasua na kifungo Dkt. Mashinji
Katibu mwenezi wa CCM Taifa amefika katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kuchukua namba ya akaunti maalumu ya serikali kwa ajili ya kulipia faini aliyohukumiwa Vicent Mashinji jana.
Mashinji ni miongoni mwa waliokuwa kwenye kesi ya uchochezi iliyokuwa ikiwakabili viongozi wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe ambapo anatakiwa kulipa Jumla ya shilingi milioni 30.
"Kulikuwa na mchakato wa ndani wa viongozi na wanachama na asubuhi ya leo tumefika hapa mahakamani kuanza kufuata utaratibu kumuchomoa ndugu yetu Mashinji na kifungo siku hili malipo ni ya kielectroniki ila tumepewa namba kwaajili ya kulipia benki na tukisharipa tutarudi hapa tupewe utaratibu baada ya hapo tutaenda gerezani kumtoa na kumkabizi kwa familia" alisema Polepole.
No comments