Maisha yana "principles". Huwezi kupata hela bila kufukia hela
Maisha yana "principles". Huwezi kupata hela bila kufukia hela. Huwezi kupata mazao bila kufikia mbegu. Huwezi kupokea bila kutoa.
Na bahati mbaya sana unaweza ukatoa na usipate. Ukafukia na usivune. Mtihani wa kwanza ukitaka kujiajiri ni kujiuliza swali moja tu! Unaweza kufukia hela bila kupata presha? kama huwezi kuwa 10% "entrepreneur". Yaani 90% ajira-10% biashara. Kumbuka uzima kwanza. Biashara zipo tu. Kama upo unaishi utazikuta tu njiani. 😂
Wanaotafuta madini "mineral explorers" wanapima ardhi kabla ya kuchimba.
Lakini pamoja na kupima, wanaweza wakachimba na wasipate. Au wakapata "kiduchu". Angali wanatumia shillingi bilioni 1 kwa siku kutafuta hiyo "gesi au hayo madini". Lakini wakikosa hawaachi.
Wanaenda pengine kutafuta. Wanaunguza tena hela nyingine. Lakini siku wakipata huo mkondo wa "dhahabu" au "mafuta" au "gesi" maisha yanabadilika muda huohuo. Unaweza ukawa umejaribu mara 10 na umeunguza pesa. Haujapata "mkondo". Usichoke! KEEP GOING! Kugundua "channel" ya hela ni siku moja TU. Lakini ukishagundua, maisha yako yanabadilika hapohapo.
@abdulnjaku
No comments