Chama Aaga Morocco, Akwea Pipa
Kiungo kutoka nchini Zambia, Clatous Chotta Chama, @realclatouschama ameposti kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram akieleza kuwa anaondoka nchini Morocco na kuwa anakwenda nyumbani.
Chama, kiungo wa zamani wa Simba ambaye amekuwa akitajwa kuwa katika mipango ya kurejea klabuni hapo, hajaweka wazi juu ya safari yake hiyo kama anaelekea Zambia au anarudi Simba.
Kiungo huyo anaichezea RS Berkane lakini kumekuwa na taarifa zisizo rasmi kuwa hana furaha kikosini hapo kutokana na kutokuwa na uhakika wa namba na mazingira ikiwemo chakula kutokuwa mazuri kwake.
Unamshauri nini Chama arudi Simba au aendelee kukomaa Morocco?
No comments